2. KATIKA
Neno katika hutumiwa kuonyesha mahali.
1. Mahali ndani au mahali eneo. Kwa mfano:
a) Watoto wameingia katika darasa lao.
b) Tutampeleka katika uwanja acheze.
c) Mimea imeota vyema katika kitalu chetu.
d) Tutasoma katika chuo kikuu cha Nairobi.
3. 2. ‘katika huonyesha hali
fulani
Kwa mfano:
1. Yuko katika fikra nyingi
2. Sitaki kuwa katika shida.
3. Katika kumsaidia mzee huyu, alijeruhiwa.
4. Barabara hiyo iko katika ubovu, haipitiki.
4. 3. ‘ katika’ hutumika kuonyesha
wakati.
Mifano katika sentensi:
1. Timu yao ilifungwa mabao mengi katika
kipindi cha pili.
2. Maria aliozwa akiwa katika mwaka wake wa
nane shuleni.
3. Aliiimba katika uzee wake.
4. Katika sherehe ya siku ya kuzaliwa kwake, rais
alimletea zawadi.
5. 4. ‘katika’ hutumiwa kuonyesha
kati ya
Mifano katika sentensi:
a) Katika matunda haya utachagua yapi?
b) Katika ng’ombe wakowatano ni yupi hutoa maziwa
mengi.
c) Katika kalamu hizi kumi napenda hizi mbili.
d) Katika masomo haya nalipenda somo la Kiswahili.
6. ‘KWENYE’
Hili ni neno ambalo hutumiwa kuonyesha:
Mahali
Mifano katika sentensi:
1. Gari lilikwama kwenye matope.
2. Simba alijificha kwenye msitu huo.
3. Tulitazama kandanda kwenye runinga.
4. Weka fedha hizo kwenye mfuko wako.
5. Mbuzi ametorokea kwenye msitu wa Mau.
‘kwenye’ huonyesha hali
1. Hapa ni kwenye furaha riboribo.
2. Kusoma kwenye ufanisi kunahitaji bidii.
3. Kutembea kwenye manufaa kwa mwili ni huko kwa utaratibu.
7. Kiambishi tamati ‘ni’
Hutumika kama ‘katika’ na ‘kwenye’ kuonyesha ‘ndani
ya’
Mifano katika sentensi:
1. Tumo mkutanoni.
2. Maji yamepunguka kisimani
3. Peleka magazeti makabatini.
4. Barabarani kuna magari mengi.
5. Watoto wanacheza uwanjani.
8. TANBIHI:
Ikumbukwe vyema kuwa ‘katika’, ‘kwenye’ na
kiambishi tamati ‘ni’ ni maneno ambayo yanaweza
kubadilishana nafasi katika sentensi. Kwa mfano:
1. Mkulima ameenda shambani
Mkulima ameenda katika shamba.
Mkulima ameenda kwenye shamba.
Katika, kwenye na -ni hivi ni vihusishi.
9. Kosoa sentensi zifuatazo:
1. Sasa ameingia kwa shuleni.
2. Mimi ninajua kwenye anaishi.
3. Nawashukuruni wote kwa kunichagua.
4. Tumemsindikiza akaingia katika garini.
10. Eleza matumizi ya maneno
yaliyokolezwa.
a) Nimemwona akiwa kwenye fikra nzito.
b) Gari liko katika mwendo mzuri.
c) Kwenye soko kuna mboga anuwai.