1. UANDISHI WA MATANGAZO
Matangazo ni habari za kijamii katika vyombo vya habari kwa lengo la kushawishi au kutoa
taarifa kwa jamii ili kununua, kuuza au kupata taarifa iliyokusudiwa kwa muhtasari. Matangazo
hulenga watu mahsusi kwa jamii
Dhima za matangazo katika jamii
Kutangaza bidhaa mbalimbali
Kutoa tahadhari kabla ya tukio linalokusudiwa kutekelezwa siku za usoni
Kuelimisha jamii – hutumika kama kutoa ujuzi, stadi, maarifa mbalimbali: mfano;
kuhusu UKIMWI, Malaria, Kipindupindu n.k
Kusaidia kuboresha shughuli za kiuchumi
Mambo muhimu katika uandishi wa matangazo
Kichwa cha habari (kuandikwa kwa herufi kubwa)
Kufanya aina ya biashara (kama matangazo ya biashara)/ aina za bidhaa
Mahali inapopatikana hiyo bidhaa au huduma
Kufanya njia ya mawasiliano
UANDISHI WA MATANGAZO MAGAZETINI
Vitu vya kuzingatia
Kutilia mkazo dhumuni la tangazo hilo
Kutumia lugha rahisi yenye sentensi fupi zenye tamathali za semi na mbinu nyingine za
kisanaa
Kutumia vivumishi vyenye kuvutia na kushawishi walengwa
Kutumia lugha ya kibunifu
Mfano wa matangazo
2. UANDISHI WA INSHA ZA KISANAA
INSHA- Ni kifungu cha habari chenye aya moja au zaidi. Insha hizo zinaweza kuwa za kisanaa
au zisizo za kisanaa.
Insha za kisanaa-Hizi ni Insha ambazo hutumia vipengele mbalimbali vya fasihi katika
kuwasilisha ujumbe. Mfano nahau, methali, misemo au tamathali za semi huweza kutumika
Mfano wa Insha za kisanaa
Mzee toboa mpenda haki
-Mzee toboa ni dereva wa teksi kwa miaka mingi jijini Dar es Salaam kutokana na uzoefu wa
kazi yake, Uaminifu, Uzungumzaji na Ucheshi kwa wateja wake aliweza kujipatia chumo nono
la kila siku. Wenzanke walimwonea gere mzee huyo, maana hata anapokuwa katulia katika
kundi la madereva akisubiri abiria wa kukodi teksi wengi humtaka yeye. Alikuwa na Umri wa
miaka arobaini au hamsini hivi, mwenye Umbo la wastani si mnene wala si mwembamba aidha
si mrefu wala mfupi kichwa chake hakikuwa kikubwa lakini kilijaa busara. hulka njema na
hekima yake kubwa vilimfanya aheshimiwe na watu.
Japokuwa hakusoma sana, mzee Toboa alijaliwa kuijua siasa ya nchi yake barabara. Alikuwa na
tabia ya kuongea na kila mtu, watoto, vijana,wazee, viongozi matajiri na makabwela, kwa
maneno mengine mzee Toboa alikuwa mcheshi na mwema. Kwa tabia yake hiyo aliweza kujua
matukio mbalimbali mitaani kwa urahisi zaidi. Yeye hakupenda Uovu wala dhuluma. Alisubiri
kwa hamu siku ambapo maovu yangetoweka kabisa .
Mzee Toboa aliweza kukemea watoto wenye tabia mbaya kwani aliweza kuwaambia Asiyesikia
la Mkuu huvunjika guu, kwa maana kwamba Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu.
Mzee Toboa aliweza kufanikiwa kujua kila Ovu lililokuwa likitokea kwani aliweza kuchukua
hatua harakaharaka.